Categories

 

September 2017
M T W T F S S
« Jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
Share |

Balozi wa Ujerumani ajitambulisha kwa Kikwete

RAIS Jakaya Kikwete amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Ujerumani, Klaus-Dieter Brandes.

Mara baada ya kupokea hati hizo Ikulu Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alifanya mazungumzo na Balozi Brandes.

Kikwete alishukuru kwa misaada thabiti ya Ujerumani hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo ya miundombinu, maji, afya, mazingira na uchumi.

Balozi Brandes kwa upande wake alimhakikishia Rais Kikwete ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa karibu na kusimamia misaada zaidi katika utekelezaji wa vipaumbele vya Serikali.

Kabla ya kuhamishia kituo chake cha kazi hapa Dar es Salaam, Balozi Brandes alikuwa Abu Dhabi na Umoja wa Falme za Kiarabu

Leave a Reply

 

 

 

You can use these HTML tags

<a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>